Monday, August 5, 2013 BIG BROTHER AFRICA: UPWEKE WAMUANDAMA FEZA
Inaoenekana upweke mkali unamuandama Feza Kessy baada ya mpenzi wake
Oneal kutoka jana kwenye shindano la Big Brother Africa, The Chase.

Asubuhi ya leo Feza ameonekana akiwa na upweke wa kufa mtu na kuuchapa
usingizi wa pono huku kitanda kilichozoea watu wawili kikionekana
kupwaya. Kuondoka kwa Oneal kunamwacha Feza peke yake hasa kwakuwa mara
nyingi alikuwa akitumia kuwa pembeni ya ubavu wa Mtwasna huyo.
Jana baada ya Oneal kupigwa kibuti na BBA, Feza alielekea juu na kukaa
mwenyewe huku akibubujikwa na machozi baada ya kuanza kuukosa uwepo wa
Oneal.
Kwakuwa Oneza imekufa rasmi jana, nani atakuwa karibu tena na Feza?
Ataweza kuendelea na mchezo huo wa kufukuzana aka The Chase mwenyewe?
Ama siku zake ndio zinahesibika?
Kwa upande mwingine, jana Uganda iliamua kutompigia kura Feza na kumpa
kura yake Bimp. Waganda wanasema wamefanya hivyo makusudi kulipiza
kisasi.
“When LK4 and Denzel were evicted where was team EAC? Denzel had to get
votes from south africa instead. Uganda does not owe anyone and anyways
this isnt a game of regionalism for Pete’s sake,” anasema Vuyolwethu
Vema Ndlovu.
“Plus Denzel was the best rep from EA this year and they didn’t support
him and they want Uganda to be loyal,” anasema Danny Lanzy.
Ogwado La Quintus Joachim wa Makerere University anasema: U Tanzanians
put LK4 N DENZEL up for eviction.. What r u talking about.. N it was
only SA tht stood with us evn with LK4 and KYLE.. We hv always been
loyal to u.. While u continuously stab us in the back.”